Artist: AIC Chang’ombe Choir (CVC)
Title of the song: USIKU WA MANANE
Duration: 7:52
Genre: Gospel
Released Year: 2024
DOWNLOAD
Download Mp3/Audio Here
USIKU WA MANANE Lyrics By AIC Chang’ombe Choir (CVC)
Kuanguka usiku wa manane kuna mateso usiku wa manane
Kuinuka usiku wa manane kuna neema usiku wa manane
Usiku wa manane usiku mtulivu (Shetani)
Anavyoutumia kuleta huzuni (mateso)
Wagonjwa wengi sana huzidiwa (usiku wa manane)
Na tena wengi wao hufariki (usiku wa manane)
Na hata wizi mwingi hufanyika (usiku wa manane)
Na mauaji mengi ya kutisha (usiku wa manane)
eeh (usiku wa manane)
eh iyee (usiku wa manane)
Uuuh (usiku wa manane)
Usiku wa manane usiku wa pekee (shetani)
Anavoutumia kuchafua hewa (mateso)
Vikao vya wachawi hufanyika (usiku wa manane)
Tena ni wakati wa mazindiko (usiku wa manane)
Makaburini nako matambiko (usiku wa manane)
Uchafu mwingi sana hufanyika (usiku wa manane)
Usiku wa manane usiku mtulivu (Jehova)
Anavyoutumia kuleta amani (furaha)
Kuzama kwa maombi ukimwita (usiku wa manane)
Ukitafuta uso wake Bwana (usiku wa manane)
Utaiona mbingu iko wazi (usiku wa manane)
Uwepo wake Bwana umejaa (usiku wa manane)
Usiku wa manane usiku wa ajabu (JEHOVA)
Huzungumza nae kila amwitae (furaha)
Na huo ndio muda wa kutubu (usiku wa manane)
Kujitakasa mbele zake MUNGU (usiku wa manane)
Na kumweleza kikusumbuacho (usiku wa manane)
Majibu ya maombi utapata (usiku wa manane)
Paulo na Sila walimwona BWANA
Walimwona (usiku wa manane)
Walikuta (milango ya gereza)
Iko wazi (usiku wa manane)
Wanawali watano wenye busara
Walimwona (usiku wa manane)
Bwana harusi (usiku wa manane)
Walimwona (usiku wa manane)
Usiku wa manane usiku wa Baraka
Usiku wa manane ni usiku wa Sifa
Usiku wa manane usiku wa Neema
Usiku wa manane usiku wa Ushindi